Karibu kwenye dalali.digital – mahali unapoweza kupata au kutoa huduma kwa haraka, kwa urahisi, na kwa uaminifu.
Tunajua kupata mtaalamu, mali au hata fundi si jambo rahisi. Mara nyingi, unahitaji mtu wa kati – dalali – ili kukuunganisha. Sisi tumeamua kulifanya hilo kuwa rahisi na la kidijitali kabisa.
dalali.digital ni jukwaa la kidijitali linalowawezesha watu:
- Kutafuta au kutoa huduma kama kazi, ufundi, usafirishaji, elimu, uhasibu, ukalimani, afya, usafi, clinics, urembo, upambaji, chakula, picha, MC, DJ, huduma za kisheria, huduma za kimtandao na zaidi.
- Kupata mali kama mali zisizohamishika, usafiri, bidhaa za vyumbani na zidi
- Kuokoa muda kwa kutumia teknolojia badala ya kutafuta mitaani.
Kwa kifupi: tunaunganisha watu bila longolongo.
Karibu uitumie. Karibu uiamini. Karibu uipendekeze kwa wengine.